Vipaumbele vya JK na Malengo ya Milenia
Kwa mujibu wa rais Kikwete, kuna mambo 11 ambayo atayasimamia kwa ukaribu zaidi katika kipindi cha miaka mitano kama atachaguliwa kuwa Rais.
Raia anasema vipaumbele vyake vitakuwa ni kuwa na taifa lenye umoja, amani na usalama na kuendelea kuimarisha Muungano, kujenga misingi ya uchumi wa kisasa kwa kuleta mapinduzi ya kilimo, ufugaji, uvuvi na viwanda, kuongeza jitihada za kuwawezesha kiuchumi wananchi wa hali ya chini, kuifanya Tanzania kuwa lango kuu la biashara na usafirishaji kwa nchi za Afrika Mashariki, Kusini na Kati, kuongeza jitihada za kuhakikisha taifa linanufaika na rasilimali za asili za nchi, kuboresha elimu ya msingi na sekondari na kupanua elimu ya ufundi na elimu ya juu na kuboresha na kupanua huduma muhimu za jamii hasa za afya maji na umeme, miundombinu ya mawasiliano na fedha.
Vipaumbele vingine ni kuimarisha utawala bora, utawala wa sheria na demokrasia, kuipa dola na vyombo vyake uwezo mkubwa wa kupanga mipango ya kiuchumi na kusimamia uchumi wa nchi kwa ufanisi, kulinda mafanikio yaliyofikiwa katika nyanja zote tangu uhuru, kuimarisha mahusiano baina ya Tanzania na majirani zake na mataifa mengine duniani pamoja na taasisi mbalimbali za kimataifa na kuendelea kutafuta marafiki wapya kwa manufaa ya taifa.
SASA KAMA UNAPENDA NCHI YAKO KURA YAKO UTAITUPA NA KUBAHATISHA RAIS?
No comments:
Post a Comment